Unknown Unknown Author
Title: Kidumu: Wakenya Wanadhani Mimi Mtanzania,Kutokana Na Kolabo Zangu Na Wasanii Wa Tz
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamuziki kutoka nchini Burundi, Kidumu, amefunguka kwa kusema kuwa Wakenya wengi wanadhani kwamba yeye ni Mtanzania kutokana na kuonyesha...

Mwanamuziki kutoka nchini Burundi, Kidumu, amefunguka
kwa kusema kuwa Wakenya wengi wanadhani kwamba yeye
ni Mtanzania kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa
wakuimba kwa lugha ya Kiswahili.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya kazi na Lady jay dee
ameiambia BBC Ijumaa hii kuwa yeye ni Mburundi lakini
kuwa karibu na Watanzania kumemfanya aonekane na yeye
ni Mtanzania.
.
“Tanzania ni nyumbani pia, nilikuwa nikienda Tanzania kila
mwisho wa mwezi, hata Wakenya wengi wanadhani mimi ni
mtu wa Tanzania, walikujakujua baadae kama mimi ni
Mburundi, lakini kwa sababu ya Kiswahili changu bado
wanasema mimi ni Mtanzania” alisema Kidumu.
Pia muimbaji huyo alizungumzia mpango mpya wa kufanya
kazi na wasanii wa Tanzania.
.
“Mpango upo kwa sababu nilishauanza, niliimba na Lady
Jaydee, niliimba na Peter Msechu wote ni Watanzania, na bado na
mpango wa kufanya kolabo zaidi,” alisema Kidumu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top