Uongozi wa label ya ‘WCB’ umesema umejipanga kikamilifu
kudhibiti swala la nidhamu kwa wasanii wake.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, mmoja
kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Babutale amesema
wao kama uongozi watasimama kidete kuhakikisha wasanii
wa WCB wanakuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.
“Nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba, sisi ni
vijana ambao tunaishi na vinaja ambao wametoka kwenye
familia zao ambazo zinamalezi tofauti tofauti, lakini wakija
hapa ni lazima wafuate sheria zetu. Sitaki kumsifia Dioamond
ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa
wengine lazima wafuate tabia za kaka yao,” alisema Babu
Tale.
Aliongeza, “Kwetu msanii akitukana kwenye social network ,
akitukana kwenye stage huyo lazima sisi tumuadhibu. Kuna
adhabu ambayo inasukumwa na social network hiyo
hatuizingatii kwa sababu kila mmoja ana mapenzi yake na
wengine wanachuki zao. Adhabu ambayo tatizo linaonekana
wazi kwamba hili ni tatizo, tunayaita matendo kusudi, kiofisi
huwenda mtu akasimamishwa bila jamii kujua, kukata pesa
kwenye kazi zake bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia
hata sisi viongozi pale tunapokosea.
Post a Comment