Mwanamitindo Hamisa Mobeto amewataka wazazi
kuuwaacha watoto kike/wakiume waingie kwenye fashion na
kuachana na dhana ya kwamba kufanya modeling ni uhuni.
Hamisamobetto amesema hayo wiki hii wakati akitoa maoni
yake juu ya nini kifanyike ili kuboresha tasnia ya mitindo,
Hamisa amewataka wazazi kuichukulia tasnia ya fashion
.
“Unajua Watanzania wengi bado hawajajua nini maana ya
modeling , wengine wanadhani ni uchafu, uhuni,” alisema
Mobeto. “Tanzania kuna Wanawake wazuri sana, kama
wazazi wakiwaruhusu vijana wao kufanya modeling basi
Tanzania tutafika mbali sana kwa sababu tuna warembo
wengi sana,”
.
Pia mrembo huyo ameitaka serikali kuangalia tasnia ya
fashion ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana wengi
pamoja na kuitangaza nchi.
Post a Comment