Unknown Unknown Author
Title: Vifafa Vyamrudia Tena Lil Wayne,Ndege Binafsi Aliyokuwa Amepanda Yalazimika Kutua Kwa Dharura
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Lil Wayne ameshambuliwa tena na vifafa. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ndege binafsi aliyokuwa amepanda rapper huyo, ililazimika kutua kwa dh...



Lil Wayne ameshambuliwa tena na vifafa.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ndege binafsi aliyokuwa
amepanda rapper huyo, ililazimika kutua kwa dharura huko
Omaha, Nebraska Jumatatu hii. Weezy alikuwa akisafiri
kutoka Milwaukee kwenda California pindi tukio hilo
lilipotokea.

Wayne alidaiwa kuzimia akiwa kwenye ndege na kupewa
huduma ya kwanza. Hata hivyo ripoti zimedai kuwa alikataa
kutibiwa. Taarifa zimedai kuwa alipata tena kifafa cha pili
baada ya ndege yake kupaa na ililazimika arudishwe Omaha.
Alipoteza kabisa fahamu na alipelekwa hospitali kwa
ambulance.

Tunechi aliwahi kupata tatizo kama hilo mwaka 2012 baada
ya ndege binafsi kutua kwa dharura kwa siku mbili mfululizo.
Pia aliwahi kupata kifafa kikali mwaka 2013.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top