Msanii wa Uganda , Eddy Kenzo alimuandikia wimbo maalum uitwayo kwa jina lake ‘Shilole’
Muimbaji huyo ameiambia Bataz kuwa Kenzo ni mtu anayempenda tangu zamani japo haimanishi kwamba ni wapenzi.
“Eddy Kenzo nadhani nilikuwa Nigeria akanicheck, ilikuwa zamani sana. Ni kaka tu ambaye alikua na mapenzi na mimi. Mpaka mtu alifika stage ya kuandika wimbo kwaajili yangu, ni mtu ambaye ana mapenzi” Amesema
“Ni wimbo wenye feeling mzuri lakini sio kusema kwamba ni mpenzi wangu kama mnataka iwe hivyo, tutaangalia” ameongeza
Hivi karibuni, Shilole aliachana na mpenzi wake wa miaka mitatu, Nuh Mziwanda kutokana na sababu ambazo hajaziweka wazi.
Post a Comment